Psalms 127

Bila Mungu, Kazi Ya Mwanadamu Haifai

(Wimbo Wa Kwenda Juu. Wa Sulemani)


1 a Bwana asipoijenga nyumba,
wajengao hufanya kazi bure.
Bwana asipoulinda mji,
walinzi wakesha bure.

2 bMnajisumbua bure kuamka mapema
na kuchelewa kulala,
mkitaabikia chakula:
kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake.


3 cWana ni urithi utokao kwa Bwana,
watoto ni zawadi kutoka kwake.

4 dKama mishale mikononi mwa shujaa
ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.

5 eHeri mtu ambaye podo lake
limejazwa nao.
Hawataaibishwa wanaposhindana
na adui zao langoni.
Copyright information for SwhKC